Michezo

Cristiano Ronaldo asaini mkataba mpya na Real Madrid mpaka 2018

Cristiano Ronaldo amesaini mkataba mpya utaomfanya aichezee Real Madrid hadi mwaka 2018 mkataba ambao unamfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi nchini Hispania kwa kupokea kiasi cha Euro milioni 17 kwa mwaka pamoja na kupewa haki ya 60% ya matangazo na zinazo baki zitaenda Real Madrid.

article-0-1AE9098B000005DC-200_634x592

Hata hivyo, sasa ataongeza asilimia hizo, japokuwa klabu nayo imebaki na haki zake pamoja na kuhakikishiwa kupata faida za kiuchumi kutoka kwa uwekezaji utaofanywa kutokana na kutumika kwa fedha zitakazotengenezwa na matangazo ya Cristiano Ronaldo.

Rais wa Real Madrid Florentino Perez na Cristiano Ronaldo walikuwa na majadiliano ya muda mrefu, lakini hatimaye wakafikia mwisho kwa maelewano na kufuta tofauti zao zilizokuwa msimu uliopita.

“Kila kitu kipo sawa kwa sasa, wamekuwa na maelewano mazuri,” walisema watu wa karibu wa pande zote mbili.

Real Madrid imepanga kutangaza mkataba huo mpya na Ronaldo kabla ya kuanza kwa ligi hapo Agosti 17 ingawa inaonyesha mkataba huo mpya si kwa sababu ya fedha pekee, lakini ni mapenzi pia na kwasasa atapata ulinzi wa rais wa klabu , klabu yenyewe, wachezaji wenzake pamoja na mashabiki ,kwamujibu wa chanzo hicho cha habari.

Florentino anataka kuhakikisha Cristiano Ronaldo anabaki Real Madrid hadi atakapostaafu kama ilivyokuwa kwa Jorge Mendes, ambaye sasa ni wakala wa wachezaji.

Ni Mendes ambaye alifanikiwa kumshawishi Cristiano Ronaldo kukubali kuondoka katika klabu hiyo kwa sababu hakuna klabu bora duniani zaidi ya Real Madrid. Hata hivyo, Samuel Eto’o amebaki kuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi duniani kwa sasa akifuatiwa na Ronaldo anayeongoza kwa Hispania pamoja na Messi.

Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents