Burudani

Kassimu Mganga na Nyota Ndogo katika radio/tv yako

Msanii wa Bongo Flava, Kassimu Mganga ametangaza kolabo na msanii Nyota Ndogo kutoka nchini Kenya.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Somo’ amebainisha hilo katika mahojiano na Planet Bongo ya EA Radio na kusema October Mosi mwaka huu ataenda Nairobi kwa ajili ya kushoot video.

“Nimekamilisha albamu lakini naaza kushoot baadhi ya nyimbo walau kwenye albamu kuwe na video walau tano, kwa hiyo tarehe moja nasafiri kwenda Kenya kushoot video, pia na kolabo na nyota ndogo nafikiri hiyo ndiyo inanipeleka huko,” amesema Kassimu Mganga.

Iwapo kolabo hiyo itakamilika na kutoka jiandae kupata muziki nzuri kupitia radio na tv yako kwani utakuwa ni mchanganyiko wa muziki wa aina mbili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents