Michezo

Kevin Prince Boateng atangaza vita nchini Italia ‘Pengine mimi ndio Cristiano Ronaldo wa Sassuolo’

Kevin Prince Boateng atangaza vita nchini Italia 'Pengine mimi ndio Cristiano Ronaldo wa Sassuolo'

Baada ya kukamilisha usajili wa miaka miwli ndani ya klabu ya Sassuolo ya Italia, Kevin Prince Boateng ametangaza vita na mshambuliaji hatari duniani, Cristiano Ronaldo.

'Am I the Cristiano Ronaldo of Sassuolo? Maybe yes..' Boateng told SkySportsItalia recently

Kufuatia ujio wa Ronaldo kwenye ligi ya Italia, kumemfanya mchezaji, Prince Boateng kupongeza zoezi hilo akiamini kuwa uwepo wa mshambuliaji huyo bora kabisa duniani atawezesha Serie A kuwa na ushindani mkubwa huku akiuliza je yeye ni Cristiano Ronaldo wa Sassuolo na kujijibu mwenyewe kuwa pengine ikawa hivyo.

Since joining Sassuolo, Boateng has been in fine form, scoring five goals in two matches

Je mimi ni Cristiano Ronaldo wa Sassuolo, pengine ndio lakini nina magoli 500 tu. Nahitaji kumshinda lakini chakwanza lazima uishinde Juventus ambao wanawachezaji wengine waliyo bora.

Kwa upande wangu siwezi kumshinda Ronaldo peke yangu ninahitaji msaada wa wachezaji wenzangu. Usajili wake unaonyesha kwakiasi gani ligi hii ya Serie A ilivyo na umuhimu, yeye ni mchezaji bora duniani na amekuja hapa  ninaamini tutapata faida ya uwepo wake kwa vitu ambavyo havijapata kuonekana Italia.

Ronaldo joined Boateng in moving to Italy this summer after finalising a £100m Juventus move

Mchezaji huyo mwenye asili ya Ghana amesajiliwa Sassuolo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Frankfurt nchini Ujerumani huku mpaka sasa akiwa ametupia mabao matano kwenye michezo yake miwili aliyocheza yakirafiki ya kujiandaa na msimu mpya waligi.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents