Habari

Kilo 78 za dawa za kulevya aina ya Heroin zapelekea watu watano kuhukumiwa adhabu ya kifo huko Vietnam

Mahakama ya Vietnam imewahukumu watu watano adhabu ya kifo baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya aina ya heroin nchini humo.

heroin

Shirika la habari la nchi hiyo limesema wanaume watatu na wanawake wawili wamehukumiwa adhabu ya kifo huko Bac Giang, Vietnam kwa kukutwa na kilo 78 za dawa za kulevya aina ya Heroin, na watu wengine wanne wiki iliyopita walikutwa na hatia kwa kosa kama hilo. Mpaka sasa idadi ya watu 500 waliokutwa na hatia ya kujihusisha na biashara ya ‘unga’ wako katika foleni ya adhabu ya kifo kwa makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya nchini humo.

Biashara ya dawa da kulevya inaonekana kushamiri kwa kasi katika nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, ambayo siku chache zilizopita raia wake wawili wasichana walikamatwa nchini Afrika kusini na karibia kilo 150 za dawa za kulevya aina ya Crystal methamphetamine zenye thamani ya zaidi ya shilling billion 6.

SOURCE: SABC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents