Tia Kitu. Pata Vituuz!

Lupita Nyong’o asimulia alivyonyanyapaliwa kwa weusi wake “Mdogo wangu aliitwa mrembo kisa mweupe ” – Video

Lupita Nyong'o asimulia alivyonyanyapaliwa kwa weusi wake "Mdogo wangu aliitwa mrembo kisa mweupe " - Video

Lupita Nyong’o asimulia namna alivyokua akitambulika kwa weusi wake tangu alipokua mdogo Kenya. “Mdogo wangu wa kike alikua akiitwa mrembo kwasababu yeye si mweusi sana kama mimi. Nilijiona sina thamani”, anasema Lupita.

Anasema kumtambua mtu kwa rangi yake kuwa mweusi sana au mweupe sana ni mwanzo wa ubaguzi wa rangi. Anaongeza kuwa inasikitisha hayo yanatokea katika nchi zetu ambapo wengi zaidi ni weusi.

Muigizaji aliyeshinda tuzo ya Oscar alizungumza wakati akifanya mahojiano na  BBC Newsday kuwa ukoloni sio wa kiutawala tu bali hata ubaguzi wa rangi na kuongeza kuwa katika “ulimwengu unaofadhili ngozi nyepesi juu ya ngozi nyeusi”.

Ikumbukwe Nyong’o alizaliwa na alilelewa Kenya, kabla ya kuhamia nchini Marikani.

Nyongo Alisema kuwa dada yake mdogo, ambaye ngozi yake ilikuwa nyepesi, aliitwa “mrembo” na “mrembo” kauli hizo zilinifanya nijione Sistahili’

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW