Bongo Movie

Mad Mad Entertainment yawaletea ‘neema’ wasanii wa Bongo Movies

Yasmin

Wasanii wa Bongo Movies wana nafasi ya kuongeza wigo wa kazi zao katika soko la kimataifa baada ya kampuni ya Mad Mad Entertainment ya nchini Uingereza kuanzisha mchakato wa kupeleka wasanii wa tasnia hiyo nje ya nchini.Lengo la mpango huo ni katika jitihada za kuikuza tasnia hiyo nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bi. Yasmin Razak kwa muda mrefu aliokaa nchini Uingereza hajaona kama kuna maendeleo kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Razak alisema ndio maana ameamua kuanzisha mradi huo ili kuikuza sanaa hiyo.

“Katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila kazi itakayouzwa hapa nchini,” alisema.

“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema Tanzania nao kuingia katika mchakato huo.”
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.

Source; Michuzi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents