Siasa

Mahujaji waendelea kusoteshwa na ATC

SERIKALI imeingilia kati sakata la kukwama kwa mahujaji wanaokwenda Makka na kuamua kutafuta suluhu ya dharura ya kuwasafirisha kwa awamu mbili, wakati siku ya leo ikiwa ndiyo ya mwisho.

SERIKALI imeingilia kati sakata la kukwama kwa mahujaji wanaokwenda Makka na kuamua kutafuta suluhu ya dharura ya kuwasafirisha kwa awamu mbili, wakati siku ya leo ikiwa ndiyo ya mwisho.


Taarifa za uhakika kutoka serikalini zinaeleza kuwa hatua hiyo ilikuja baada ya mahujaji waliokuwa wasafirishwe na ATC kushindwa kuondoka hadi kufikia jana usiku baada ya kukosekana ndege kwa zaidi ya wiki moja, hali iliyozusha malalamiko kutoka kwa mahujaji hao.


Inadaiwa kuwa hatua ya ATC kushindwa kuwasafirisha mahujaji hao, iliishitua serikali na hatua ya juzi usiku ya mke wa Rais, Salma Kikwete, kwenda kuwafariji mahujaji hao akitokea Dodoma alikokwenda kuhudhuria maadhimisho ya miaka 46 ya uhuru ilitokana na hali hiyo.


Mke wa Rais alifika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na akawataka kuendelea kuwa na subira wakati serikali ikifanya kila linalowezekana ili waweze kusafiri.


Wakati mahujaji hao wakisubiri hatima yao, juzi usiku Nyang’anyi ambaye ni Mwenyeki wa Bodi ya ATC, aliwaambia mahujaji mbele ya Salma kuwa, ndege ya kuwachukua iliyokodiwa kutoka Saudia ilikuwa njiani ikielekea Dar es Salaam ambako ilitarajiwa kufika wakati wowote na kuwachukua mahujaji 379 wa kwanza, ahadi ambayo hadi jana saa 2:00 usiku ilikuwa haijatimia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents