Mitindo

MAONYESHO YA NNE YA SWAHILI FASHION WEEK YAZINDULIWA

founder_of_Mustafa_Hassanali_Speaking_face

 

Swahili Fashion Week ambayo ni maonyesho makubwa Afrika Mashariki na Kati, yakiwa  mwaka kwenye wake wa nne yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa  tarehe 10, 11 na 12 mwezi wa Novemba 2011 Dar es Salaam, Tanzania.


Swahili Fashion Week 2011 itawaleta pamoja wabunifu 50 wa mavazi na vishaufu kutoka nchi ziongeazo Kiswahili na nchi nyingine mbali mbali kuonesha ubunifu wao wa hali ya juu na kuonesha mitindo mipya ya mavazi.

“Kwa mwaka huu tumekua maradufu kwani tuna jumla ya wabunifu 21 waliobobea kutoka Tanzania, wabunifu 10 wanaochipukia kutoka Tanzania, na waliosalia wanatoka katika nchi mbali mbali duniani na kwa ujumla wao wanakua wabunifu 50, ambao watakao jiunga na watanzania wote kusherehekea miaka 50 ya UHURU wa nchi yetu.” Alisema Mustafa Hassanali, Mwanzilishi wa maonyesho ya Swahili Fashion Week.

 

founder_of_Executive_Secretary_of_The_National_Arts_Council_Ghonche_Materego_unveiling_the_new_logo_of_Swahili_Fashion_Week_2011during_the_press_conference_of_the_Launch_of_Swahili_Fashion_week_at_Southern_Sun_29th-9-2011

Pamoja na kuwa na maonyesho ya ubunifu wa mavazi kutakua na Maonyesho ya Manunuzi ya bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa Tanzania yalioyoanzishwa mwaka 2010, kwa mara nyingine maonyesho haya yatakua kivutio kikuu katika Swahili Fashion Week. Mpaka hivi sasa, maonyesho haya yana washiriki 30 waliojisajili kushiriki, nahii inafanya maonyesho haya kua maonyesho makubwa nchini.

founder_of_Sponsorsfounder_of_Swahili_Fashion_Week_Mustafa_Hassanali_and_the_Exective_Secretaryof_Basata_Ghonche_Materego_watching_power_point_presentation_of_participating_Designers_of_Swahili_Fashion_week__29th-9-2011
Kama tulivyokua wa kwanza kuanzisha Maonyesho ya mavazi kama haya, kwa mara nyingine tena tanakua wa kwanza kuanzisha tuzo katika sekta hii ya ubunifu Afrika ya Mashariki na Kati. Kusheherekea mafanikio yaliyofikiwa katika sekta hii ya ubunifu wa mavazi. Kutakua na Mashindano ya Ubunifu wa Fulana ambayo pia ni ya kwanza, kama njia ya kuwashirikisha vijana na vipaji vyao kama njia ya kukuza sekta hii ya familia hii ya wabunifu.


Founder_of_Swahili_FashionWeek_Mustafa_Hassanali_with_the_Executive_Secretary_of_The_National_Arts_Council_Ghonche_Materego_on_the_Press_Conference_of_the_Launch_of_Swahili_Fashion_week_at_Southern_Sun_29th-09-2011
Pia kuna matukio mbali mbali yanayoandaliwa na na yatafanyika kulekea  kwenye maonyesho haya ya Swahili Fashion Week. Kwa kuanza kutakua na maonyesho ya mavazi jijini Arusha ambayo ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 8 mwezi Oktoba 2011 kama njia moja wapo ya kupelekea na kusambaza kazi za ubunifu katika mikoa mingine ya Tanzania.

Swahili Fashion week 2011, itakua inarushwa hewani moja kwa moja kupitia tovuti ya www.swahilifashionweek.com kuwapatia fursa wanahabari wa ubunifu duniani kote na kuwajulisha yanayojiri katika ulimwengu wa ubunifu Afrika Mashariki. Maonyesho haya ya moja kwa moja kutoka Makumbusho ya Taifa yatawapatia fursa Watanzania waishio ughaibuni nafasi ya kuunganika na Watanzania wote katika kusheherekea miaka 50 ya UHURU.

“Tukiwa na malengo ya kukuza biashara hii ya ubunifu katika ukanda huu, ninapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru washirika wetu wote, waliotudhamini katika miaka iliyopita mpaka wakati huu, na pia tungependa kuchukua fursa hii kuhamasisha makampuni na mashirika mbali mbali kujitokeza na kutuunga mkono kwa kudhamini maonyesho haya ya Swahili Fashion Week” Alimalizia Mustafa.

Swahili Fashion week 2011 imedhaminiwa na Nyumba ya Swahili Fashion Week – Hoteli ya Southern Sun, EATV & East Africa Radio, Precision Air, BASATA (Baraza la Sanaa Taifa), Amarula , Ultimate Security, REDDS Original, Image Masters, Global Outdoor ltd, Vayle Springs ltd, Eventslites, Nipashe, Perfect Machinery ltd, Michuzi blog, PKF Tanzania and 361 Degree.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents