Michezo

Mashabiki wa United wahamishia hasira zao kwa Sanchez, mwenyewe aomba yaishe

Nyota wa Manchester United, Alexis Sanchez amejikuta akifuta picha na video zake za matangazo ambazo ameziposti muda mfupi tu tangu kufanya hivyo baada ya kukabiliwa na maneno ya karaha, kejeli na dharau kutoka kwa mashabiki wa United.

Sanchez leo siku ya Jumatatu aliposti picha zinazotangaza nguo zake mpya kupitia mtandao wake wa Twitter na hivyo mashabiki wa United kumjia juu kwa kumuandikia ujumbe wenye karaha, kejeli na dharau kutokana na kufanya kitendo hicho saa chache wakati klabu yake ikitoka kupokea kipigo cha mabao 3 – 2 dhidi ya Brighton mchezo wa ligi kuu England.

Mchezaji huyo wazamani wa Arsenal raia wa Chile aliposti picha na video zinazomuonyesha akiwa amevalia aina hiyo mpya za nguo zake akiwa sambamba na JJO.

The advert focuses on Sanchez's toned physique, especially his ripped abdominal muscles 

Mchezaji huyo anayelipwa zaidi ligi kuu England amejikuta akiingia kwenye matusi ya hali ya juu kutoka kwa mashabiki ”Tumemsajili mwanamitindo tunayemlipa 350,000 kwa wiki,” maneno ya mashabiki wa United wakihamishia hasira ya kipigo cha ligi kuu kwa nyota huyo ambaye jana usiku hakucheza kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Sanchez received criticism from fans for posting the ads so soon after United lost to Brighton

Related Articles

2 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents