Soka saa 24!

Mbwana Samatta kutimkia La Liga ya Hispania, aandaliwa dau nono 

Mbwana Samatta kutimkia La Liga ya Hispania, aandaliwa dau nono 

Klabu ya Levante inayoshiriki ligi kuu ya nchini Hispania Laliga inahaha kuhakikisha inapata saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ili kuimarisha kikosi chao kwa maandalizi ya mashindano mbalimbali.

Klabu hiyo kutoka nchini Hispania imetenga kitita cha euro milioni nne ili kumsajili Samatta lakini klabu yake anayo itumikia kwa sasa KRC Genk ya Ubelgiji imekataa ofa hiyo na kuhitaji euro milioni nane.

Wakala wa Samatta amethibitisha kuwepo kwa mazungumzo baina ya klabu hizo mbili huku miamba ya Urusi klabu ya CSKA Moscow imekuwa ikihitaji huduma ya kijana huyo Mtanzania.

Mbwana Samatta lipojiunga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji mwezi Januari mwaka 2016 akitokea katika miamba ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW