Michezo

Video: Msikiti unaotembea wazinduliwa kwenye michuano ya Olympic Japan

Video: Msikiti unaotembea wazinduliwa kwenye michuano ya Olympic Japan

Wenyeji wa michuano ya Olympics mwaka 2020 nchi ya Japan imeamua kujidhatiti kuelekea mashindano hayo yanayo shirikisha mataifa mbalimbali kwa kutengeneza magari yenye misikiti ambayo itaweza kutembea kila mahali ili kuwapatia huduma ya kusali wageni wote watakao hudhuria.

Kwamujibu wa scoopempire.com Magari hayo ambayo yametengezwa na Tokyo company yamezinduliwa mapema wiki hii kwaajili ya kuonyesha wageni wenye imani ya dini ya Kiislamu watakao hudhuria kwenye mashindano hayo makubwa.

Kutokana na chombo cha habari cha Euronews kimeripoti kuwa Magari hayo yenye ‘air-conditioned’ yatakuwa na uwezo wa kuingiza watu 50 kila moja ambao watapata nafasi ya kusali huku ikitumika teknolojia ya simu kubaini kibla ambapo ni mahala patakatifu kwa dini ya Kiislamu Maka.

Inaelezwa kuwa hapakuwa na mpango wowote kwa watu kufanya ibada maeneo ya uwanja wa taifa wa Tokyo ndipo mfanyabiasha mmoja akaja na wazo la kuwepo kwa Misikiti hiyo maeneo hayo ili kusaidia waumini wa dini ya Kiislamu kufanya ibada.

Nchi hiyo bado inaendelea na mipango hiyo ya kutengeneza aina hiyo ya Misikiti iliyopewa jina la ‘mobile mosques’ kwaajili ya mashindano ya Olympics na Paralympics itakayo anza kufanyika Julai 24 hadi Agosti 9 mwaka 2020 kwenye jiji la Tokyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents