Michezo

Mchakato wa mabadiliko wa Yanga na Mafanikio yake – Farhan Kihamu, Sehemu ya Pili

Tunaendelea na sehemu ya pili kuhusu uwekezaji na mpira kuhamia kwa Wafanyabiashara, Vijana, Matajiri na watu mashughuli duniani!

Swali la kwanza linasalia kwa nini YANGA kwenye mchakato wa mabadiliko walitumia model inayotumika nchini Hispania? Kila nchi Ulaya ina muundo wake wa Utawala wa mpira na uwekezaji, ukienda England wana fit-and-proper-person test (nitawapa darasa lake) Ukienda Ujerumani wana 50 +1.

Yanga wameenda Hispania ambapo wana Sociedad Anónima Deportiva’ (S.A.D.) model, hili pia nitawapa darasa lake siku nyingine kwanini WAHUNI wanasumbua nayo, ukifeli kwenye model maana yake umefeli kwenye muundo mzima wa uwekezaji na utawala, cha kwanza kwa Simba ianze kwenye muundo kisha ndipo iendelee, sehemu ambapo tumekwama muda wote.

BILIONEA MO Dewji ama GSM wanaweza kuwa wanatoa pesa sana kwa ajili ya klabu lakini pesa zinaenda wapi? Zinatumika vipi na kwa muundo gani? Hapa ndipo ulipo utofauti wa Simba na Yanga, unarudi kwenye setup, mfumo, watu wa mfumo, matamanio ya watu wa mfumo na malengo yao, mfumo uliopo sasa hauibebi Simba kwakuwa mpira umebadilika (evolving).

TAJIRI MO DEWJI anapitia njia ambayo Tajiri mwingine TAMIM BIN HAMAD AL THANI huyu ndie Mmiliki wa PSG kupitia Qatar Sports Investment na yule Bwana Mdogo Nasser El Khelaffi pale ni Mtu wake wa karibu akampa asimamie projects zake akiwa amemtoa kwenye kampuni zake, lakini licha uwekezaji mkubwa sana bado PSG haijashika soka la Ulaya, ikalazimika wabadili mfumo wao.

PSG wakaona ipo haja ya kuwa na watu wanaofahamu soka la Ulaya vyema, simu ikapigwa kwa Akili ya Kireno mtu ambaye ana thamani kubwa Ureno baada ya Cristiano Ronaldo, Luis Figo, Eusebio na Jose Mourinho, Mwamba anaitwa LUIS CAMPOS ama THE WIZARD OF THE CAPITAL GAIN.

Campos huyu Mwanaume aliipa Ulaya ile Monaco hatari ya wakina Bernado Silva, James Rodriguez, Bakayako na wengine akatisha sana Ulaya kisha akaenda kubeba Ubingwa na Lille kwa gharama nafuu sana (nikitulia nitawapa visa vyake)

Mmiliki wa PSG hakuamini kama Makocha pekee ndio tatizo, aliamini kwenye eneo la UTAWALA kunahitaji mabadiliko, ndipo akamtambulisha Luis Campos kama Mkurugenzi wa mpira…..

 

 

 

 

 

INAENDELEA…
Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents