Tia Kitu. Pata Vituuz!

Mchezaji wa Juventus akutwa na Virusi vya Corona

Klabu ya Juventus imetangaza kuwa mchezaji wake, Daniele Rugani amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Image result for daniele rugani

Klabu hiyo ya ligi ya Serie A imesema kwamba imechukua hatua zote za kumtenga mchezaji huyo zinazohitajika kisheria ikiwemo kuwashirikisha wale ambao waligusana naye

Klabu hiyo imeongezea kwamba Rugani mwenye umri wa miaka 25 kufikia sasa hajaonesha dalili za ugonjwa huo.

Michezo yote nchini Italia imeahirishwa hadi Aprili 3 huku taifa hilo likijiweka katika karantini kutokana na mlipuko huo wa coronavirus.

Beki huyo wa kati ameichezea klabu yake mara saba pekee msimu huu na hakutumika katika mechi ya Juventus dhidi ya Intermilan ambayo klabu hiyo iliibuka na ushindi wa 2-0 katika mechi iliochezwa bila mashabiki siku ya Jumapili.

Mechi ya Inter iliotarajiwa kucheza dhidi ya Getafe katika michuano ya Europa siku ya Alhamisi pia imeahirishwa.

Rugani ameshinda mataji manne ya ligi ya Italia akiichezea Juventus na aliichezea Italia mara saba, mara ya mwisho ikiwa 2018.

Siku ya Jumapili alichapisha picha mtandaoni katika chumba cha maandalizi cha Juve akisherehekea ushindi wa klabu hiyo dhidi ya Inter pamoja na wachezaji wenzake.

Italia imerekodi visa 12,000 vya maambukizi na vifo 827 kutokana na virusi hivyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW