Mfahamu mmiliki wa Wasafi TV ambaye ndiye muandaaji wa tamasha la Fiesta
Ni miezi kadhaa sasa imepita tangu kituo kipya cha runinga cha Wasafi TV kianze kurusha matangazo yake hewani, huku kukiwa na mkanganyiko mkubwa kwenye jamii juu ya mmiliki mkubwa wa kituo hicho.
Sintofahamu ya mmiliki hasa wa kituo hicho, ilikuja baada ya baadhi ya watu kudai kuwa mmiliki ni Diamond Platnumz wengine wakidai kuwa mmiliki ni Joseph Kusaga, ambaye ni Ofisa Mtedaji wa Clouds Media Group.
Swali ni Je, ni nani haswa mmiliki wa Wasafi TV?
Kampuni ya Clouds Media inajishughulisha zaidi na biashara ya burudani, kupitia tamasha la Fiesta ambalo lipo chini ya Primetime Promotions, kusimamia wanamuziki na studio za kurekodi muziki kupitia THT.
Kwa upande mwingine, Kampuni ya Wasafi pia nayo inamiliki lebo ya muziki ya WCB, Studio za kurekodia muziki Wasafi Records, Vyombo vya habari kama Wasafi FM & Wasafi TV, platform za kusambaza nyimbo mtandaoni Wasafidotcom na pia kampuni hiyo ndio waandaaji wa tamasha la Wasafi Festival.
Mzozo uliopo kati ya Media hizo, unaonekana kupuuzwa na baadhi ya watu, hii ni kutokana na ukaribu mkubwa uliopo kati ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Clouds Media, Joseph Kusaga na C.E.O wa Wasafi, Diamond Platnumz.
Ukaribu wa Diamond na Kusaga, ndio uliopelekea watu wengi kuhisi kuwa huenda DJ huyo wa zamani ana hisa zake ndani ya Wasafi TV. Mpaka sasa Clouds FM na Clouds TV hawapigi nyimbo za wasanii wote wa WCB, jambo ambalo linazidi kuchochea uhasama.