Burudani ya Michezo Live

Mfahamu mpiga mbizi mwenye uwezo wa kuzama kwenye kina kirefu bila chombo chochote alivyonusurika kufa – Video

Mfahamu mpiga mbizi mwenye uwezo wa kuzama kwenye kina kirefu bila chombo chochote alivyonusurika kufa - Video

“Watu huniuliza: ‘unaweza kutafakari maisha bila kupiga mbizi?’ Nawajibu: ‘Unaweza kuishi bili kula?'” Herbert Nitsch alilelewa katika nchi ya Austria ambako hakukaribiani na maji, lakini anavutiwa na maji kama samaki.

Amevunja rekodi ya kupiga mbizi kina kirefu bila kutumia kifaa maalum cha kumsaidia kuvuta pumzi.

Ana uwezo wa kujizuia kuvuta pumzi kwa dakika tisa na kupiga mbizi hadi mita 253 chini ya maji.

Pia aliongelea kuhusu upendo wake wa kuogelea na kupiga mbizi- na jinsi karibu apoteze uhai wake.

Mtindo wa kupiga mbizi uitwao ‘No limits’, huelezwa kuwa mtindo wa hatari sana , ambapo mpiga mbizi huzama chini umbali mrefu, na kurejea juu ya uso wa maji akiwa na boya.

Njia hii ni hatari sana hata wenye utaalamu na upigaji mbizi wanakiri hivyo kwani pia wapiga mbizi kadhaa wamepoteza maisha.

Herbert Nitsch akipiga mbizi

Ni mtihani mzuri wa uvumilivu na ujasiri kwa wapiga mbizi kama Nitsch.

Lakini ni changamoto ambayo imemuandaa kwa miaka yake mingi ya mafunzo na mashindano

Kupitia mbinu mbali mbali, ameripotiwa kuongeza uwezo wake wa mapafu hadi lita 14 – wastani kwa mwanaume ni karibu lita sita.

Mnamo Juni 2007 Nitsch alishuka hadi mita 214 kuweka rekodi mpya ya ulimwengu.

Mnamo mwaka wa 2012, alienda zaidi, akitokea kwa mita 253 karibu na Santorini huko Ugiriki.Hivi ndivyo alivyoelezea uzoefu wake ambao karibu ugharimu maisha yake.

“Nilifunga macho yangu na sikugundua chochote karibu yangu. Ulimwengu wa nje haukuwapo.”

Katika mita 15 alisimama kutoa hewa yake kuelekea ndani ya chombo cha EQUEX (equalization extension tool) – kitu kama chupa ya plastiki iliyokazwa zaidi na bomba juu na shimo chini.

Alitengeneza chombo hiki kusawazisha shinikizo ndani ya mwili wake wakati wa kupiga mbizi chini zaidi – kutofaulu kufanya hivyo kunaweza kusababisha majeraha kama kupasua ngoma ya masikio.

Herbert Nitsch akiwa kwenye boti

Ninaposhuka zaidi, navuta hewa kidogo kidogo. Tatizo ni kuwa ukiwa kwenye kina kirefu huwezi kupata hewa kutoka kwenye mapafu tena.

Hata hivyo, ninapovuta hewa ndani ya chupa hizi.

Bado ninaweza kupata hewa kwa kina. Kubana pumzi yangu yote ndani ya EQUEX inachukua kama nusu dakika.

Bado Herbert Nitsch aliweza kuvunja rekodi yake mwenyewe na akaenda chini kwa mita 253.

Lakini kurudi kwake juu ya uso wa maji kumeonekana kuwa na shida. Akiwa njiani kurudi alipotea kwa sababu ya hali inayoitwa nitrogen narcosis, hali ya kuchoka iliyosababishwa na gesi fulani

Narcosis wakati mwingine huitwa “athari ya martini” – Mpigambizi anapozama kina kirefu zaidi huhisi hali ya ”ulevi”.

Kujihisi umelewa

Unapokwenda kina kirefu zaidi unalewa kutokana na gesi ya naitrojeni. Unajihisi umelewa kabisa, hii hali ya kulewa ilinifanya nipate usingizi nikiwa umbali wa mita 80.”

Herbert Nitsch kwenye boti

”Katika mita 26 wapigambizi wa kikosi cha uokoaji walinipata.”

Kwa hofu kuwa Nistch amepoteza fahamu kutokana na kukosa hewa, timu ya usalama wa majini ilimpeleka nchi kavu haraka.

Lakini aliamka baada ya kufikishwa nchi kavu, alijua alichotakiwa kufanya.

Kupoteza fahamu

Nitsch alifikishwa hospitalini mjini Athens, alikini alipoteza fahamu kabla ya kufika hospitalini.Madaktari walianza kumhudumia haraka, lakini waliiambia familia na marafiki kuwa anaendelea vizuri.

Herbert NitschKupiga mbizi kwenye kina kirefu kunaweza kusababisha vifo
Mpiga mbiziShinikizo ndani ya maji linaweza kusababisha kusinzia

Leo ni miaka saba, Nitsch amepona kwa kiasi kikubwa. lakini bado ana hajaweza kupiga mbizi kweye kina kirefu kama awali, lakni hufanya hivyo kwa kuwa anaupenda mchezo huo. ”Ninapokuwa ndani ya maji kila kitu kiko sawa.Ndani ya maji ninajihisi kama mtoto”.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW