Technology

Microsoft yauza kilichobaki Nokia kwa kampuni nyingine

Baada ya kutumia gharama kubwa mwaka 2014 kuinunua Nokia, Microsoft imeamua kuiuza kwa kampuni ya Foxconn kwa dola milioni 350.

shutterstock_171217538_Nokia-730x368

Kwenye dili hiyo kampuni tawi la Foxconn, FIH Mobile Ltd. Itakichukua kiwanda cha simu cha Microsoft kilichopo Vietnam. Microsoft pia inaigawa brand ya Nokia na mambo mengine.

Hiyo haimaanishi kuwa Microsoft inajiondoa kabisa kwenye utengenezaji wa simu – itaacha tu kutengeneza vifaa vya Nokia.

Katika maelezo yake, Microsoft inasema itaendelea kutengeneza Windows 10 Mobile na kusupport simu kama Lumia 650, Lumia 950 na Lumia 950 XL, na simu za kampuni rafiki ya OEM za Acer, Alcatel, HP, Trinity na VAIO.

Hivi karibuni Microsoft ilipunguza wafanyakazi 8,000 kutoka kwenye idara yake ya simu na kuziachia dola bilioni 7.6 ilizozitumia kwenye Nokia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents