Burudani

Mimi sio mtu wa kiki, kiki zinanifuata zenyewe – Harmorapa

‘Kiboko ya Mabishoo’ Harmorapa amefunguka kwa kudai kuwa yeye siyo mtu wa kupenda kiki kama baadhi ya watu wanavyodai kupitia mitandao ya kijamii.

Rapa huyo amekuwa akitawala mitandao ya kijamii kila kukicha kutokana na vituko vyake huku watu wakidhani huenda akawa anapanga kufanya matukio ya namna hiyo ili azungumziwe kwenye vyombo vya habari.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Harmorapa amedai vitu vingi anavifanya katika hali ya kawaida lakini vinakuzwa na media hali ambayo amedai kwake haoni kama ni tatizo.

“Nawaona sana watu wanavyosema mimi ni mtu wa kiki, lakini mimi siyo mtu wa kiki, kiki zinanifuata zenyewe,” alisema Harmorapa.

“Mimi naweza kufanya kitu cha kawaida ambacho hata msanii mwingine anaweza kufanya lakini cha kushangaza, kwangu kitaonekana ni kitu kikubwa sana. Kwa hiyo mimi naona ni kutokana na jinsi watu wanavyonichukulia lakini siyo kwamba natengeneza kiki,”

Rapa huyo amedai tayari ameshaanza kuona mwanga katika maisha yake ndani ya kipindi kifupi toka aanze muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents