Michezo

Mourinho anafuata nyayo za Ferguson – Eric Cantona (Picha)

Mchezaji wazamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Eric Cantona amesema kuwa anavutiwa mno na falsafa ya meneja, Jose Mourinho na kutokana na kushinda mataji makubwa ndani ya msimu mmoja tu uongozi wake anafuata nyayo za Sir Alex Ferguson.

Mchezaji wazamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Eric Cantona

Cantona raia wa Ufaransa amecheza Old Trafford miaka ya 1992 na 1997 amemtaka Mourinho kutwaa mataji mengi zaidi akiwa kama meneja wa United.

Eric Cantona amekiri kupata tabu kuelewa kwa nini Mourinho anapata matokeo mabovu katika mechi za ligi kuu Uingereza.

Kupitia mahojiano na  FullTimeDEVILS, Cantona amesema “United sikuzote hucheza vizuri na kufurahia mchezo hata enzi za Sir Matt Busby ilikuwa ni falsafa ya timu. Ubunifu katika mchezo, pasi na kuhakikisha unasonga mbele lakini pia kushinda ilikuwa ni jambo muhimu.” Amesema Cantona

Cantona akifanyiwa mahojiano na watangazaji channeli ya FullTimeDEVILS  Stephen Howson (kulia) na Adam McKola (kushoto)

 

“Mourinho atashinda kilakitu na United na mpenda Mourinho. Ni kama Barcelona endapo ikicheza kwa kujilinda hakuna atakaeipenda. Kwa United falsafa hiyo ni imara ijapokuwa kwa sasa kuna ugumu kidogo kuielewa.”

Mourinho ameshinda ubingwa wa EFL Cup na UEFA Europa League ndani ya msimu wake wa kwanza akiwa United kitu ambacho kinaleta matumaini ya kufikia mafanikio ya kocha wazamani, Sir Alex Ferguson.

Cantona ameisaidia United kutwaa mataji manne ya ligi ya Uingereza, mawili ya FA Cup katika misimu yake mitano ndani ya klabu ikiwa ni pamoja na ubingwa wa ligi mbili kwa wakati mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents