Habari

Msajili wa Vyama vya Siasa aionya Chadema kwa kuongeza ubeti wa tatu kwenye wimbo wa Taifa (Video)

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi ameionya CHADEMA kutokana na alichokiita uvunjifu wa sheria kwa kuongeza ubeti wa tatu kwenye wimbo wa Taifa
https://www.instagram.com/p/CDdpPMPBBHq/
Ameeleza kuwa kitendo hicho kilifanywa jana wakati Baraza Kuu la CHADEMA lilipokuwa likimpendekeza atakayepeperusha bendera ya Chama hicho katika nafasi ya Urais

Msajili amesema, “Nimesikitishwa na kitendo cha kuvunja sheria kwa makusudi kilichofanywa na CHADEMA cha kuchukua wimbo wa Taifa na kuongea aya”

Amesisitiza, “Kwa hili ambalo limefanyika na CHADEMA ni kama kunajisi wimbo wa Taifa. Nataka kuwaonya wakati wanaendelea na mikutano yao, waheshimu sheria za nchi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents