Bongo Movie

Mtoto wa King Majuto ‘Hamza Majuto’ kuwainua wasanii wachanga wenye vipaji

Mtoto wa mchekeshaji nguli katika tasnia ya filamu na vichekesho nchini Tanzania, King Majuto, Hamza Majuto chini ya “Hamza Majuto Film” yupo kambini akiandaa filamu mpya yenye waigizaji chipukizi kwa lengo la kuwainua na kuwawezesha kujimudu wenyewe kwenye kazi zao za sanaa.

“Nimeingia kambini na waigizaji chipukizi ili niwasaidie kupitia kampuni yangu waweze kujitegemea wenyewe kwenye kazi zao,” Hamza ameiambia Bongo5.

Pia amesema kuna kazi waliyofanya yeye na baba yake Mzee Majuto wakimshirikisha JB ambayo inatarajia kuingia sokoni siku za hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents