Technology

Mwanasheria Alberto Msando aeleza jinsi sheria ya makosa ya mtandaoni itakavyowapeleka jela wanaopenda kutukana Instagram

Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amesema sheria mpya ya makosa ya mtandaoni itakula kwa wengi.

11376214_107263722941646_889752710_n

Msando ameiambia Bongo5 kuwa utekelezaji wa sheria hiyo si mgumu kama wengi wanavyodhani na infact wengi wataenda jela. “Ili sheria itekelezeke huhitaji kushtaki watu wote,” amesema Msando. “

“Huwezi ukakamatwa wewe umemtukana Albert ukasema na Abdalah alimtukana naye akamatwe. Ukikamatwa wewe tunaanza na wewe. Kwahiyo ukimuona mwenzio amefungwa miezi sita, miaka saba, miaka mitano, amelipishwa faini, definitely utaacha.”

“Kwasababu kazi ya sheria ni kwanza kumrekebisha mtu kwa njia ya adhabu na pili kumsababisha mtu aepuke kufanya jambo kitu fulani. Inapopitishwa ukiona watu wa kwanza wa pili kweli imetekelezeka, kuna watu wataacha zile tabia maake watajua sasa hapa ni tatizo. Na umeangalia kabla hata haijatumika watu wanakuambiwa ‘tutukane ya mwisho mwisho kabla ya hiyo sheria haijaanza kupitia. Tayari watu wameshajua ni makosa kufanya mbili tatu.”

Msando amewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuheshimiana na kuitumia kwaajili ya maendeleo na kupata taarifa sahihi.

“Mimi nimeitumia vizuri, nimepata wateja zaidi ya watano wa kazi kubwa tu kwa kupitia mitandao ya kijamii.”

Msikilize hapo chini.

Kama wewe ni mpenzi wa mitandao ya kijamii na unaitumia vyema kwaajili ya kuchat na washkaji, Tecno Boom J7 ni simu inayokufaa. Jipatie sasa kwa shilingi 250,000 tu.

Unaweza pia kujishindia Boom J7 mpya kwa kufollow ukurasa wa Instagram wa Tecno Mobile Tanzania. Ni rahisi sana. Bofya hapa na uende kufollow ukurasa wa Instagram wa Tecno Mobile Tanzania unaweza kuwa mmoja wa watu watakaoshinda.

Kwa taarifa zaidi like ukurasa wa Facebook wa Tecno Mobile Tanzania hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents