Burudani

Ndoto ya Wema Sepetu kuwa mbunge yayeyuka!

Haikuwa bahati yake. Safari ya Wema Sepetu kuelekea bungeni imefikia tamati.

11373808_714714575320591_607196619_n

Hiyo ni baada ya kushindwa kuwashawishi wanachama wa CCM mkoani mkoani Singida kumpa dhamana ya kuwawakilisha kwenye viti maalum vya ubunge.

Wema ameshindwa kupita kwenye kura za maoni za ubunge huo kwa kupata kura 90 tu. Aliyeongoza kwenye kinyang’anyiro hicho ni Aysharose Mattembe (311), Martha Mlata (235) na Diana Chilolo (182).

Wema amekubali kushindwa na kudai kuwa ushiriki wake umempa ujasiri zaidi.

“Nilivyoamua kugombea viti maalum, nilijua kuna kupata na kukosa. Awamu hii nimekosa, ila dunia bado inazunguka,” ameandika kwenye kwenye Instagram.

“Nawapongeza walioshinda. Nawashukuru mlioniunga mkono, Mungu aendelee kuwabariki kwa mapenzi yenu juu yangu, yananipa moyo. Nawashukuru pia wote mlionipinga maana mmeniongezea ujasiri na nina nguvu mpya ya kuthubutu upya,” ameongeza.

“2015 ni mwaka wa kipekee kwenye muamko wa vijana Tanzania. Bigger things loading.. Most of all Nilizaliwa nikiwa katika Chama Cha Mapinduzi na nitakufa nikiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi…. Safari yangu ya Siasa ndo kwanza inaanza.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents