Soka saa 24!

New Video: Mr. Kesho – Nangoja

Staa mpya anazaliwa, japo jina lake Mr Kesho linaweza kuonekana kuukata ustaa wa leo. Wimbo wake Nangoja, umewashtua wengi na wale wenye maskio makali zaidi ya muziki mzuri, wamebaini ndani ya Kesho, kuna dhahabu itakayoanza kumwagika yenyewe bila hata kuchimbwa.

https://www.youtube.com/watch?v=dcpzbyOkiHY&feature=youtu.be

Ni uthibitisho tosha kwanini label ya Dropouts Entertainment iliamua kutupa karata zake kwake. Nangoja umetayarishwa na Taz, gwiji wa utayarishaji wa muziki kutoka Zambia, aliyejipatia jina Tanzania kwa kuupika wimbo wa Fid Q, Walk it Off na kuimba kiitikio chake.
Muimbaji huyo sasa anaachia video ya wimbo huo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu.

Ilimpasa kukwea pia na kwenda Nairobi, Kenya kuitafuta quality hii kutoka kwa muongozaji mjuzi, X Antonio, anayefahamika kwa kuongoza video za thamani za wasanii wakubwa wa Kenya zikiwemo Olalo ya Papa Dennis aliyomshirikisha rapper wa Senegal, Sarkodie, Usiogope ya Timmy aliyomshirikisha DNA na Ndathima ya Jimmy Gait.

Wazo la video hiyo limetoka Dropouts Entertainment huku script ikiandikwa na muigizaji wa filamu wa nchini Zambia na mshindi wa tuzo kibao, Cassie Kabwita.

“Hii ni video tofauti sana, ” anasema Mr. Kesho. “Ni video ambayo tumejitahidi kubuni kitu kipya katika macho ya watu hivyo nategemea itapokelewa vizuri sana na Watanzania, nina imani itafanya poa sana, kikubwa mnisupport tu,” ameongeza. Nangoja ni wimbo wa mapenzi unaoelezea subira aliyonayo mwanaume ya jibu toka kwa msichana anayempenda.

“Nimemu-approach msichana ambaye amenizidi uwezo, uzuri, nyota, amenizidi kila kitu ndio nikawa nasubiria jibu langu, ndio ikawa hiyo Nangoja,” amefafanua.

Ubora na upekee wa video ya Nangoja, unaupa nguvu zaidi wimbo huu na kuuongezea sifa za kuchezwa na kuonekana kwenye vituo vya runinga vya kimataifa na kumweka Mr Kesho kwenye orodha ya wasanii wa kuwaangalia zaidi Afrika mwaka 2017. “Uwezo wake wa kuandika kila aina ya muziki, kupokea criticism to positivity, uwezo wake wa kuufuatilia muziki wa Afrika na dunia kwa ujumla unatia moyo,” wanasema Dropouts Entertainment kuhusu Mr. Kesho. “Ana kipaji kikubwa, pia ni mtu humble sana. To us he is the next Africa legend and we feel happy working with the next African legend.”

KUHUSU MR. KESHO

Salum Said aka Mr. Kesho ni msanii aliyesainishwa na label mpya ya muziki nchini, Dropouts Entertainment. Jina lake la muziki alipewa na marafiki zake baada ya kuwa wakimuuliza kwanini hatoki kimuziki licha ya kuwa na kipaji kikubwa, na jibu lake lilikuwa lilelile ‘Nitatoka Kesho’ na hivyo kubatizwa rasmi na mtaa kwa jina ‘Mr. Kesho.’

KUHUSU DROPOUTS ENTERTAIMENT

Ikiwa na mtazamo mpya wa namna ya kuendesha biashara ya label za muziki, Dropouts Entertainment imedhamiria kuleta mapinduzi nchini Tanzania. “Malengo yetu ni kuwa big publisher wa kazi za wasanii kupitia technology and to invest kwa new generation yenye kiu ya mafanikio,” inasema. Hadi sasa wasanii walio chini ya label hiyo ni Mr. Kesho, na Linah Sanga, ambaye miradi yake mipya itaanza kutoka baadaye mwaka huu.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW