Bongo Movie

Ney wa Mitego:JB hana tofauti na Wema, Aunty Ezekiel

Msanii ‘controversial’ nchini, Ney wa Mitego jana amemuangushia bomu muigizaji wa filamu nchini, Jacob Steven aka JB kuwa hana tofauti na waigizaji wa Bongo Movies anaowachukulia kama vicheche.

Kauli hiyo ameitoa jana kwenye kipindi cha Hot Mix cha EATV baada ya hivi karibuni kukwaruzana na JB jijini Mwanza kwenye ziara ya Fiesta. Inadaiwa kuwa Ney alimwita Wema kicheche jukwaani jambo lililomfanya muigizaji huyo kukwaruzana na Ney.

“JB alikuwa kama mtoto mdogo au ulifika time wacha tu niliongee hili,” alisema Ney. Ilifika time nikasema JB simtofautishi na wale akina Aunty Ezekiel sijui akina Wema kwasababu unajua mtoto wa kike ni dhaifu unajua, mimi nilimsamehe Aunt Ezekiel na Wema pia, sababu Wema na Aunty Ezekiel ni watu waliotaka kugombana na mimi, niliwasamehe palepale. Nachokisema sio kama nabahatisha, nakuwa na uhakika nacho. JB na Ray ilibidi waungane pamoja wanifuate, ‘bwana unajua mimi ni dogo kwao’ lakini labda tunashindana tu vitu fulani, ukubwa wa umri si tatizo.”

JB na Ray

Uhusiano mbaya kati ya waigizaji wa filamu nchini na Ney ulianza baada ya rapper huyo kudai kwenye wimbo wake‘Nasema Nao’ kuwa makahaba wenye kiwango wapo kwenye Bongo movies.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents