Paulsen ataja Kikosi
Kocha huyo alifungua dimba kwa kutaja majina ya wachezaji kuwa ni Shaban Kado pamoja na Said Mhando na kipa Juma Kaseja.Wachezaji wengine ni shedrack Nsajigwa,Erasto Nyoni,Haruna Shamte,Stephano Mmasyika,Idrisa Rajabu na Juma Nyoso ambao ni mabeki.
Paulsen aliendelea kutaja viungo wengine wakiwemo Shaaban Nditi,Henry Joseph, Nurdin Bakari,Jabiri Azizi,Niza Khalifan wengine ni Meshak Ab el,Mohamed Banka pamoja na Kigi Makisi.
Kocha huyu aliwataja washambuliaji kuwa ni pamoja na Dan Mrwanda, Mrisho Ngasa, John Bocco,Thomas Ulimwengu na Gauence Mwaikimba , hivyo hawa ndio watakaocheza katika sakata hilo ambapo tayari nchi 12 , ikiwemo Tanzania , Kenya, burundi, Uganda,Rwanda, Somalia,Ethiopia, Sudan, Zanzibar na timu nyingine zilizokaribishwa ni kutoka Ivory Cost, Zambia pamoja na Malawi.
Awali Brand Meneja Breweries LTD(SBL) Tusker, Nandi Mwiyobella slisema, ’Tumeahidi kupanda kwa viwango vya wachezaji wa timu Afrika ya Mashariki na Kati, ili kuwawezesha hata kushiriki katika mashindano ya Kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazili na kusema, chapa ya Tusker ina moyo huo.
Nandi aliendea kusisitizia kuwa wakiwa kama wadhamini wakuu wa michuano ya CECAFA watahakikisha Tanzania inaweka historia na kufanya vizuri kwani wamejipanga vizuri kwenye michuano ya CECAFA.