Michezo

Pep Guardiola amfunika Jurgen Klopp, Pochettino kocha bora wa msimu, awekwa chungu kimoja na Sir Alex Ferguson na Mreno Jose Mourinho kwa hili

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola ameshinda tuzo ya kocha bora wa msimu wa 2018/19 wa Ligi kuu England (Premier League).

Pep Guardiola anafanikiwa kushinda tuzo hiyo mara ya pili mfululizo baada ya kuisaidia klabu yake ya Man City kubeba ubingwa wa Premier League na kuwashinda Jurgen Klopp, Mauricio Pochettino na Nuno Espirito Santo ambao waliingia fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.

Mbali na kutwaa tuzo hiyo ya kocha bora, Pep Guardiola ameingia kwenye rekodi ya kuwa miongoni mwa mameneja watatu waliyofanikiwa kutwaa ubingwa huo wa Premier League mara mbili mfululizo ‘back-to-back seasons’ baada ya kufanya hivyo Sir Alex Ferguson na Mreno Jose Mourinho.

Ferguson amefanikiwa kufanya hivyo akiwa na Manchester United, wakato Mreno Mourinho akiwa na kikosi cha Chelsea mara yake ya kwanza alipokuwa Stamford Bridge.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents