Soka saa 24!

Picha: Diamond azifunga barabara za Bukoba, he is a ‘celebrity’

Ni Juma Nature, Mr Nice na Profesa Jay pekee waliowahi kufurahia mafanikio na kupendwa hivi anavyopendwa Diamond sasa.

Hitmaker huyo wa Kesho yupo ziarani mikoani na huko anapokelewa kama mfalme. March 30 alikuwa Bukoba mkoani Kagera na alikutana na mapokezi ambayo hawezi kusahau maishani.

Diamond akiwa amembeba shabiki mtoto
Diamond akiwa amembeba shabiki mtoto

Kupitia website yake Diamond ameandika:

Tarehe 30 March niliwasili salama salimini mjini Bukoba mkoani Kagera, pili niwashukuru mashabiki wangu wote mkoani kwa kunipokea kwa hali na mali. Hii inaonyesha jinsi gani watanzania wanathamini na wana mapenzi na wasanii wao. Nililazimika kutoka Juu ya Gari kuwasalimu kabla sijaelekea hotelini.

Nilivotokeza hali ilizidi kuwa mbaya zaidi. Polisi walilazimika kufunga barabara kadhaa mjini bukoba na hata kazi zingine kusimama kwa muda kutokana na watu kuzingira Gari nilokuwepo kila kona nilipokuwa pita.
IMG_0300

IMG_0317

Na katika show yake watu zaidi ya 3,000 waliingia na kusababisha mwandaaji kusitisha kuuza tiketi.

IMG_0093

IMG_0145

“Nilikinukisha vilivyo kama kawaida yangu na kuweka historia mpya ndani ya Bukoba kuwa mwanamuziki wa kwanza kupiga show mwenyewe na kujaza watu zaidi ya 3,000 hadi kufikia uongozi kusitisha kuuza ticket kutokana na jeshi la polisi kutoa taarifa ingeweza kutokea maafa kama ilivyotokea kabla ya mimi kupanda jukwaani.”

Kanga Moja nao walikuwepo na kufanya yao. Kutokana na ukali wa picha hizo tumeziwekea effect.

IMG_0181

IMG_0177

IMG_0180

IMG_0179

IMG_0178

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW