Picha

Picha: Dunia yampinga Trump baada ya marufuku kwa Waislamu kuingia Marekani kuanza Jumamosi hii

Uamuzi wa Donald Trump kupiga marufuku wahamiaji wa kiislamu kutoka kwenye nchi zenye raia wengi wa dini hiyo, umesababisha hasira kuu duniani kote na wahamiaji wakikataliwa kupanda ndege kuingia Marekani.

Raia waliokuwa na hati za kusafiria kutoka Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walizuiliwa kwenye viwanja vya ndege, wakati wale waliokuwa wameshapanda ndege walishikiliwa baada ya kutua Marekani.

Katika tukio moja, abiria watano wa Iraq na mmoja wa Yemeni, waliokuwa na visa halali, walizuiliwa kupanda ndege ya EgyptAir iliyokuwa ikitoka Cairo kwenda New York na hatimaye kuelekezwa kwenye ndege zinazorudi kwenye nchi zao.

Mwanamke mmoja aliyekiambia mauaji ya Isis nchini Iraq mwaka 2014, alizuiliwa kupanda ndege mjini Baghdad, baada ya kusubiria visa kwa miezi mingi ili akaungane na mumewe ambaye tayari yupo Marekani. Rais Trump amepiga marufuku kwa miezi mitatu wakimbizi toka nchi saba duniani, ili kuchuja magaidi wa kiislamu wasiingie nchini humo.

Wakimbizi kutoka Syria wamepigwa marufuku kimoja.

Hata hivyo, jaji mmoja alitoa ruhusa Jumamosi kwa raia kutoka nchi hizio saba waliokuwa wameshaingia nchini humo, wale waliokuwa njiani, wenye visa halali kukaa Marekani. Waandamaji kadhaa walikusanyika kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani Jumamosi hii kupinga uamuzi huo wa Trump. Maandamano zaidi yatafanyika Jumapili hii.

Hizi ni picha za maandamano hayo:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents