Tia Kitu. Pata Vituuz!

Picha: King Kaka atembeza mitaani mixtape yake mpya, auza zaidi ya nakala elfu 3 ndani ya masaa matano

Biashara ya album imekuwa ni swala lenye changamoto nyingi kwa wasanii wa Tanzania kiasi cha kuwafanya wengi wasitamani kutoa album, lakini kwa mfano wa alichokifanya rapper wa Kenya huenda ikawasaidia wasanii kuwaza njia mbadala za kusambaza kazi zao badala la kukimbia jukumu la kutoa album.

kaka1
King Kaka akiwa na shabiki aliyenunua mixtape yake

King Kaka a.k.a Rabbit wa Kenya Ijumaa iliyopita aliamua kuingia mwenyewe kwenye mitaa ya jiji la Nairobi kuuza mixtape yake mpya na ya saba ‘It’s The King’. Kila nakala moja aliuza kwa shilingi 200 Ksh sawa na 4,300 Tshs. Katika zoezi hilo alifanikiwa kuuza nakala 3149 ndani ya masaa matano.

Wakati wa zoezi hilo rapper huyo pia alikuwa akipiga picha na mashabiki wake aliokuwa akikutana nao mitaani na kuzipost Instagram, kwasababu lengo lake lilikuwa kukutana na mashabiki wengi zaidi ambao hawapati nafasi ya kukutana naye ana kwa ana.

Kaka ameiambia Mseto kuwa amefurahishwa na matokeo ya alichokifanya baada ya kwenda mitaani na kuwashukuru wote wanaou-support muziki wa Kenya.

kaka5

kaka2

kaka3

kaka4

kaka6

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW