Bongo Movie

JB adai huu sio wakati wa kuwashirikisha wasanii wa nje ili kutoboa kimataifa

Msanii na mtayarishaji wa filamu Jacob Stephen ‘JB’ amesema mbinu ya wasanii wa filamu kutegemea kuwashirikisha wasanii wa Nigeria na Ghana ili kwenda kimataifa imepitwa na wakati.
Jb

Muigizaji huyo ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ‘Jerusalem Film’, ameiambia filamucentral kuwa mbinu hiyo iliwasaidia akina Kanumba kwa wakati nyuma na sio sasa.

“Hakuna haja ya kuwashirikisha wasanii kutoka Nigeria au Ghana ili kufanya filamu kubwa, Marehemu Kanumba alifanya hivyo kwa wakati ule ilikuwa wakati wake, sasa watu wanataka sinema kubwa kutoka kwetu,” alisema JB.

Pia JB alisema muigizaji mkongwe Hashim Kambi, alimleta muigizaji wa Nigeria Van Vicker na kucheza filamu ‘Never give up’ lakini haikuwa filamu kubwa.

Aidha, JB alisema anathamini mchango wa marehemu Kanumba kwa kuitangaza tasnia ya filamu nje, kwani toka kuondoka kwake hakuna aliyefanikiwa kufanya vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents