DStv Inogilee!

Picha: Shilole aingia studio Afrika Kusini kurekodi na producer wa Uhuru

Shilole a.k.a Shishi baby anaendelea kufanya maandalizi ya kuupeleka muziki wake kimataifa, kwa kufanya kazi na watayarishaji wa muziki wa nje ya Tanzania.

Shishi na Maphorisa
Shishi akiwa na Maphorisa

Baada ya kufanya wimbo na producer wa Nigeria, Selebobo mwishoni mwa mwaka jana alipoenda nchini humo, Shishi ameingia studio kurekodi wimbo mwingine na producer wa Afrika Kusini, Dj Maphorisa wa kundi la Uhuru.

“Me n my baddest producer in Africa about to do magic in the studio please follow him @djmaphorisa” ameandika Shilole ambaye yuko Afrika Kusini na Linah.

Shishi na Maphorisa-2

Maphorisa ameshafanya kazi na wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika akiwemo Wizkid, Davido, RunTown na wengine.

Baadhi ya wasanii wa Tanzania ambao tayari wamefanya kazi na producer huyo ni pamoja na Chege (Sweety Sweety) na Linah (Ole Themba).

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW