Picha: Studio ya kisasa yazinduliwa Mombasa, Kenya

Kuna wakati muziki wa kizazi kipya ulikuwa unapata changamoto nyingi hasa upande wa utayarishaji wa muziki Afrika Mashariki.

Mahali pa utayarishaji wa muziki katika studio za Victory

Wasanii ni wengi na wana uwezo mkubwa kimuziki maana vipawa vyao vinawaruhusu kufanya hivyo. Nikiwa mdau mmoja wao mimi binafsi, nimeshawahi kushuhudia kuona kazi za wasanii zikichukua muda mrefu katika utayarishaji (Production) wa muziki hivyo kuwavunja moyo baadhi ya wasanii wakiwa katika harakati za kuutengeneza muziki.

Ofisi ya kisasa kwenye Victory Music Studio

Kucheleweshwa kwa ngoma za wasanii studioni, huchangia kuua makali ya ujumbe ambao msanii huwa amekusudia kulenga hadhira maalumu kwa wakati fulani hivyo ikapelekea ngoma ikaishia kubuma.

Jiji la Mombasa limechangia kwa kina kuukuza na kuusukuma muziki wa kizazi kipya kwa kiasi kikubwa. Tokea zamani studio za muziki zimekuwa zikijikamua kutoa kazi za wasanii jinsi ziwezavyo, licha ya shinikizo la wasanii wengi wanavyozidi kumininika ili kutengeneza muziki.

Na sasa wadau wa muziki Mombasa wanafanya kila wawezavyo ili waweze kutimiza na kuzima kiu cha wasanii kwa kujenga studio za kisasa zitakazo weza kuukabidhi ushindani ulioko kwasasa Afrika Mashariki na bara zima la Afrika.

Kuna baadhi ya wasanii wakubwa Afrika Mashariki, ambao kitovu cha upenyu wao kwenye muziki ulikua jijini Mombasa. Mfano tu, Nyota Ndogo ambaye mpaka sasa bado hajatoka Mombasa, mwanadada Akothee licha ya kuwa kitovu chake ni nyanda za ziwa Victoria ama Kisumu, lakini kipawa chake cha muziki kiliibuka jijini Mombasa na wengine wengi.

Hizi ni picha za studio ya Victory Music Studio iliyopo hapa Mombasa, inatarajiwa kuziba pengo la uhaba wa studio za muziki katika Pwani ya Kenya na kuleta muziki bora zaidi kwenye soko la muziki Africa.

Makala ya: Changez Ndzai
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram: changez_ndzai

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW