Picha: Wafahamu wamasai waliyoitikisa Uingereza kwenye kriketi wiki hii
Timu ya wamasai wanaocheza mchezo wa kriketi kutokea Kenya, wameitikisa Uingereza kwa mavazi ya asili huku wakifanikiwa kucheza michezo ya kirafiki na klabu kadhaa kwenye tour yao yenye lengo la kuongeza uwelewa juu ya usawa, kuchukia uhalifu, utumwa na kutangaza utamaduni wao.
Wakiwa England timu hiyo ya Wamasai inayotokea huko Laikipia nchini Kenya wamefanikiwa kucheza na Nottinghamshire Knights, Cavaliers & Carrington pamoja na Belvoir Cricket & Country Trust siku ya Jumatano.
Katika ziara yao Uingereza kikosi hicho cha wamasai wamefanikiwa pia kuwa kabili Notts & Arnold Amateur na Attenborough Cricket Club.
Kupitia tovuti ya vijana hao wameeleza kuwa ”Lengo letu ni kuwa wezesha vijana katika jamii zetu kupitia maendeleo ya mchezo wa kriketi, ili kuwafanya kuwa wenye afya imara na kuwa wazalishaji wazuri katika jamii,” wameandika wamasai hao.
Kikosi hicho cha wamasai kimeanzishwa miaka 11 iliyopita kinatarajia kuhitimisha tour yao siku ya Jumamosi, Uingereza kwa kufanya sherehe huko Nottingham.
Timu hiyo ikiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo wakijadili mchezo wao.
Watu muim sana duniani kwakuheshim tamaduni zao ,big up masai