Burudani ya Michezo Live

Prince Harry na Mkewe wakerwa na magazeti ya Udaku ya Uingereza, wadai hawatakubali kuharibiwa maisha yao

Mwana wa Mfalme Prince Harry na mkewe wamesema katika mahojiano ya pamoja waliofanya na kituo cha televisheni cha ITV wakati wa ziara yao nchini Afrika mapema mwezi Oktoba na kurushwa hewani Jumapili, kuwa hawatakubali magazeti ya udaku ya Uingereza kuwaharibia maisha yao.

Mwana wa Mfalme Harry akiwa na mke wake Meghan.

Mwana wa Mfalme Harry akiwa na mke wake Meghan.

Prince Harry ameiambia ITV kuwa mengi ya mambo ambayo yanachapishwa katika magazeti ya udaku siyo ya kweli, akiongeza “Sitakubali kuingizwa katika hujuma iliyomuua mama yangu.”

Harry amesema ”kumbukumbu ya kifo cha Princess Diana ilikuwa bado ingaliipo kila siku kunavyokucha na sio kwamba yeye mwenye amejawa na hofu”

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Voice Of America, Nyota wa zamani wa Televisheni ya Marekani Meghan Markle amesema wakati rafiki zake walikuwa na furaha ya yeye kuwa na mahusiano na Harry, marafiki zake wa Uingereza walimuonya kuwa asiowane na Harry kwa sababu magazeti ya udaku ya Uingereza yatamuharibia maisha yake.

Akizungumza namna anavyoweza kukabiliana na ufuatiliaji mzito wa magazeti hayo, Meghan amejibu “Ukweli ni kuwa nimekuwa kwa muda mrefu nikimwambia Harry haitoshi kuwa utanusurika katika jambo, hiyo siyo maana ya maisha. Inatakiwa upate mafanikio.”

Mapema mwezi huu wana wa mfalme hao walifungua mashtaka dhidi ya gazeti la udaku la Uingereza, The Mail on Sunday kwa kuingilia maisha yao ya faragha, akidai kuwa kinyume cha sheria walichapisha barua aliyomuandikia baba yake.

Kila wakati, Harry alisema namna wanavyomfanyia Meghan hakuna tofauti na vile magazeti hayo yalivyomfanyia mama yake.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW