Shinda na SIM Account

Professor Jay afunika Sweden!!

Professor Jay in Stockholm
Mwanamuziki maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini tanzania professor jay aka wamitulinga aka dad aka joseph haule juzi jumamosi ya tarehe 6 alifanya tamasha la nguvu au watoto wa mjini wanasema tamasha la kufa mtu mjini Stockholm nchini Sweden.

Kabla ya tamasha hilo lililoweka historia mjini hapo watanzania walijitokeza kwa wingi na kwenda kumpokea airport kwa shangwe na kununua cds za album zake kama njugu. Wakati wa show hiyo Professor Jay alianza kwa kishindo na nyimbo inayopendwa sana ulaya ktk nchi za ulaya ya zali la mentali na kusababisha ukumbi mzima kulipuka kwa shangwe na vifijo.

Mashabiki hao ambao wengi wao walikuwa kutoka ukanda wa afrika mashariki waliendelea kupata burudani ya mfululizo huku wakipata free style za nguvu sambamba na nyimbo zake zinazotamba kama piga makofi, bongo dar es salaam, ndio mzee, chemsha bongo, hakuna noma, joseph nk.

Pia mwanamuziki huyo aliyeonekana kuwa amejiandaa vya kutosha aliwashangaza sana mashabiki baada ya kuimba nyimbo nyingi bila kuchoka kama vile ana mapafu ya mbwa, mashabiki hao waliokuwa wanaimba na kucheza pamoja na professor jay bila kuchoka ukumbi mzima ulilipuka na mashabiki kwenda kumtunza kwa wingi msanii huyo pale tu iliposikika kuanza instrumental au ala ya wimbo wake maarufu wa nikusaidiaje ambao mara baada ya kuuimba pamoja nao na kuisha mashabiki walimtaka aurudie na bila hiana aliurudia na kufanya mashabiki kuendelea kupagawa huku akiwaambia mashabiki kwamba amefunga safari kutoka tanzania kuja ulaya kwa ajiri yao na kwamba anaamini kwamba ni mashabiki wanaomfanya yeye awe mwanamuziki hivyo anawaheshimu sana.

Baada ya show Prof Jay alikuwa na kazi ya ziada ya kupiga picha na mashabiki lukuki ambao ilibidi wapange mstari ili kupunguza vurugu. Tofauti na wasanii wengi wanaokuja ulaya ambao hutoweka ukumbini mara tu wamalizapo show PROF JAY aliendelea kujumuika nao kufanya mashabiki wamkubali na kuridhika na ujio wake.

Pia Prof Jay ameweza kurecord wimbo nchini sweden akishirikishwa na wasanii wa kitanzania wanaoishi nchini wanaojulikana kama PLZ ambayo inawajumuisha ZIGGY LAH wa kundi la XPLASTAZ na PUZO LEE ktk studio yao iliyopo nchini Sweden inayoitwa PLZ STUDIO. Siku iliyofuata ya jumupili Prof Jay alialikwa kula chakula na watanzania wanaoishi mjini Stockholm na kubadilishana mawazo na kupiga za ukumbusho.

Prof Jay amerudi jana nchini Uholanzi na kwenda moja kwa moja kufanya interview ktk radio mbili maarufu nchini uholanzi na duniani za LIJN5 RADIO na AFRICAN HIPHOP RADIO ambapo aliweza kuutangaza vizuri muziki wake na kazi za watanzania wengine.

Msanii huyo anategemewa kufanya matamasha mengine ya nguvu katika ziara yake hii ya nchi za ulaya ambapo ijumaa hii tarehe 12 anategemewa kufanya show inayosubiriwa kwa hamu ktk ukumbi wa CLUB INTENTIONS – ROTTERDAM nchini HOLAND. Baada ya hapo yatafuta matamasha mengine mjini BERLIN – UJERUMANI, GOTHENBERG- SWEDEN, na OSLO- NORWAY.

Professor Jay European Tour imedhaminiwa na Luca ambae ni mkurugenzi wa kampuni za Mambo Jambo Entertainment na Bongo5.com.

Source: Bongo5

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW