Siasa

Rais Kikwete aahidi kuileta klabu maarufu ya Hispania nchini


Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana amesema kuwa atahakikisha anaileta klabu moja kubwa inayocheza ligi kuu ya nchini Hispania kuja kucheza mchezo wa kirafiki na timu za hapa nyumbani.
Rais Kikwete ambaye ni mpenzi mkubwa wa michezo amesema anzania ina mashabiki wengi wa timu za Hispania hususan Barcelona na Real Madrid na hivyo kama moja wapo ikija nchini mashabaki hao wataifurahia ziara hiyo.
Amesema hayo jana katika ikulu ya Dar s Salaam wakati akimkaribisha balozi mpya wa Hispania nchini, Luis Manuel Cuesta Civis.
Mazungumzo hayo yalifanyika muda mfupi baada ya balozi huyo mpya kumkabidhi rais Kikwete hati za utambulisho.
Aidha ameipongeza Hispania kwa ushindi wao wa hivi karibuni dhidi ya Italia na kunyakua kombe la Euro 2012 mwezi uliopita.
Pamoja na balozi mpya wa Hispania, jana rais pia amempokea balozi mpya wa India nchini, Debnath Shaw.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents