Soka saa 24!

Rais Magufuli akabidhiwa ramani ya uwanja mpya wa soka utakaojengwa Dodoma (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na wataalamu wa ujenzi wa uwanja wa soka unaotarajiwa kujengwa Jijini Dodoma na kukabidhiwa ramani ya uwanja wa kisasa wa mpira utakaojengwa jijini Dodoma.

2a
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane ambaye aliambatana pamoja na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco,  Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Patrick Mfugale pamoja na wajumbe wengine.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na wataalam wa ujenzi wa uwanja kutoka Morocco na pamoja na Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Abdelillah Benry.

3

Uwanja huo unatarajia kujengwa eneo la Nara Jijini Dodoma, barabara ya kuelekea Singida ambapo jumla ya hekari 143 zimetengwa. Unatarajia kugharimu Tsh bilioni 56 na ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji 85,000.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW