Habari

Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush alazimika kufanyiwa operation ya moyo

Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush jana alilazimika kufanyiwa operation ya moyo huko Dallas, Texas Marekani baada ya madaktari kugundua mishipa ya damu iliyokuwa imeziba katika moyo ‘an artery blockage’.

george bush

Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya Bush Freddy Ford , baada ya madaktari wa Cooper Clinic kugundua tatizo hilo wakati wa checkup yake ya kawaida Jumatatu wiki hii, walimshauri Bush afanyiwe upasuaji, zoezi lililofanyika Jumanne (August 6) katika hospitali ya Texas Health Presbyterian.

Katika taarifa hiyo Ford aliendelea kusema operation hiyo ilimalizika salama na sasa Mr Bush yuko katika hali nzuri kiasi cha kumfanya atamani kurejea nyumbani na kuendelea na shughuli zake za kila siku, “President Bush is in high spirits, eager to return home tomorrow and resume his normal schedule on Thursday,”.

Mr Bush mwenye miaka 67 amewahimiza watu wajiwekee utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara sababu tatizo kama lake limegundulika wakati wa checkup yake ya kawaida.

Bush anategemewa kuruhusiwa kutoka hospitali leo Jumatano na kesho ataendelea na shughuli zake.

SOURCE: REUTERS

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents