Michezo

Rasmi: Clement Sanga  ajiuzulu Makamu Mwenyekiti Yanga ‘Klabu itakabidhiwa baraza la wadhamini’

Rasmi: Clement Sanga  ajiuzulu Makamu Mwenyekiti Yanga 'Klabu itakabidhiwa baraza la wadhamini'

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga  ametangaza kujiuzulu nafasi yake ndani ya timu hiyo kongwe kabisa nchini huku sababu kubwa akidai ni maswala ya kiusalama dhidi ya mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria.

Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo Sanga amesema amejiuzulu nafasi yake Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga.

Nimejiuzulu nafasi yangu ya makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga ambayo inapelekea kuondoa nyazifa zangu zinazopeleka kuwepo kwenye klabu yetu ya Yanga.

Niwaombe radhi wale wote ambao nimewakwaza wakati wangu wa uongozi ijapokuwa mimi sikuwa msemaji sana wa vyombo vya habari.

Nafasi yangu mimi kama makamu ambayo pia nilikuwa nakaimu kama mwenyekiti klabu ya Yanga ni mali pia na malizote zina simamiwa na baraza la wadhamini kwahiyo klabu itakabidhiwa kwa baraza la wazamini.

Kunamtu ambaye ni mwanachama wa Yanga amejaribu kuongea na vyombo vya habari, kwanza hakutenda haki kwasababu anatishia familia yangu kwa maana kwamba anashawishi watu mwenye panga, mwenye jembe, mwenye shoka waje nyumbani kwangu wanapafahamu lakini bado anazungumzia Sanga yupo juu ya Serikali nikaona anatengeneza mahusiano au taswira isiyo sahihi baina yangu pia na Serikali.

 

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents