Habari

Rick Ross ashitakiwa kwa kushindwa kulipia saa (3) za Rolex zenye thamani ya karibia $ 90,000!

Swali la kwanza unaweza kujiuliza Rozay amekuwa broke? Then, to this extent?? Kiasi cha kushindwa kulipia bling zake! Big boss wa MayBach Music Rick Ross ameshitakiwa kwa kushindwa kulipia saa tatu (3) aina ya Rolex alizonunua mwaka jana.

US rapper Rick Ross

Kwa mujibu wa TMZ, duka la Johnny’s Custom Jewelry la Texas, Marekani limefungua mashitaka dhidi ya Rozay na kampuni yake ya MayBach Music, wakidai kuwa rapper huyo alikubali kununua saa 3 aina ya Rolex za Diamond mwaka jana zenye nthamani ya $89,847.50.

Risiti ya bidhaa hizo inaonesha manunuzi yalifanyika (September) 2012 na Johny’s waliufikisha mzigo kwa Rozay, lakini rapper huyo hajafanya malipo mpaka sasa, chanzo kimeripoti.

Rozay receipt

Johnny’s Custom Jewelry wanamtaka Rozay kulipia saa hizo pamoja na riba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents