Burudani

Kala Jeremiah atangaza ulaji kwa mashabiki wake wa facebook, mshindi kujinyakulia kitita cha pesa….

Mshindi wa tuzo 3 za KTMA 2013 rapper Kala Jeremiah ni kati ya wasanii wanaotumia vizuri mitandao ya kijamii katika kujiweka karibu na wadau/fans na kuzitangaza kazi zao. Jana (June 28) Kala alitangaza ulaji kwa fans wake wa facebook watakaoshinda shindano dogo alilolitoa.

kala-1

Jana ukurasa wa facebook wa hit maker wa ‘Dear God’ Kala ulifanikiwa kufikisha likes 33,333 na alipost picha ya page yake ikionesha idadi hiyo na kuwashukuru mashabiki walio-like mpaka kuifikia idadi hiyo, kisha akaahidi yeyote atakayefanikiwa kupiga picha kama hiyo pale idadi ya likes za page yake itakapofikia 44,444 na kisha kumtumia picha hiyo katika inbox yake atampatia zawadi ya Tsh 100,000 na kumtangaza kwenye ukurasa huo.

Hiki ndicho alichoandika

kala status

Hizi ni juhudi binafsi zinazotakiwa kufanywa na msanii ili kuhakikisha anajenga ukaribu na wale anaowategemea kusupport kazi zake, japo mpaka leo kuna wasanii ambao hawana akaunti facebook wala twitter, changamoto!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents