Michezo

Rundo la simu lamponza Masau Bwire uwanja wa ndege wa JK Nyerere

Msemaji machachari wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire hapo jana siku ya Jumanne alijikuta katika mtihani baada ya kutumia muda mwingi kupekuliwa uwanja wa ndege wa JK Nyerere kufuatia kukutwa na idadi kubwa ya simu wakati akihitaji kusafiri kuelekea Mbeya kwaajili ya mchezo wao wa FA unaopigwa leo dhidi ya mwenyeji Majimaji.

Msemaji machachari wa klabu ya Ruvu Shooting

Video: Masau Bwire atoa siri kutembea na rundo la simu

 

Jana, Jan 30, 2018 nilipata tabu sana uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere wakati nikisafiri kutoka Dar kuelekea Mbeya hadi Songea kwa ajili ya mchezo wa FA dhidi ya mwenyeji Majimaji mchezo utakaochezwa hii leo, Jan 31, 2018 katika uwanja wa Majimaji, mjini Songea.

Nilipekuliwa kikamilifu na wafanyakazi wa uwanja jambo ambalo japo niliona ni usumbufu, lakini niliwasifu na kuwapongeza kwa umakini waliokuwanao katika upekuzi kuhakikisha kwamba, kila anayepita na kinachopitishwa ni salama. Niliwapenda, wako vizuri!
Hayo yote sababu kubwa ilikuwa ni idadi kubwa ya simu nilizokuwanazo! Nilikuwa na simu nane na iPad moja!.

Nilipitishwa mara kadhaa katika mashine ya alarm mimi mwenyewe lakini simu zangu pia zikapitishwa mara kadhaa katika huo mtambo!
Kwa kujiridhisha zaidi, pengine mtambo unaweza kutoona mengine, wakalazimika kufanya kiafrika zaidi kwa kutumia mikono, hii yote kujiridhisha niko salama, sina makandokando kinyume cha utaratibu, yaani yale mambo ya kishetani! Hakika uwanja ule kwa ulinzi, upekuzi, watu wako vizuri, ukitaka jaribu upuuzi pita pale uone kama hatujakuandika magazetini kwa kubadilishiwa safari na usafiri, tena ukisafirishwa bure kupelekwa mahala ukahifadhiwe!.

Nilipenda zaidi pale simu moja baada ya nyingine ilipofunguliwa kuthibitisha kama ni simu kweli, huko ndani kuna line au mauzauza ya Dania hii ya wadhambi! Mtihani huu pia nikaushinda! Ya kwanza kukakutwa line ya tiGo, inapendwa sana na wanahabari kutika kunisaili. Nyingine Airtel, Voda, Zantel, TTCL, Smart, Halotel akakutana nazo mbili, zote nane zikaonekana ni salama! Hapo nikapumua, nikaruhusiwa kuketi pamoja na abiria wenzangu kama raia mwema, mtiifu kwa sheria za nchi na mwaminifu, mtu wa Mungu ninayeyapinga yote yaliyo ya Shetani!.

Ninawapongeza sana wafanyakazi wote hasa kitengo cha usalama, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere kwa kazi nzuri wanayoifanya! Pale, hakika kibovu hakipiti!.

Hongera sana, hongereni sana, kazeni uzi vivyo hivyo, watanyooka tu!.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents