Michezo

Samatta atua kimya kimya kuiuwa Malawi

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Ally Samatta tayari ametua nchini kuungana na nyota wengine katika mazoezi yanayofanyika Uwanja wa Boko Veteran, uliyopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Samatta ambaye anachezea klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji ametua nchini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi ya Oktoba 7 mwaka huu.

Katika mchezo huo ambao upo kwenye kalenda ya FIFA utajumuisha wachezaji nyota kama Simon Msuva anayekipiga nchini Morocco, mshambuliaji wa Yanga SC, Ibrahim Ajib na Mbaraka Yusuph wa Azam FC.

Taifa Stars itashuka dimbani majira ya saa10.00 jioni tayari kwa mtanange huo, Shime Watanzania kujitokeza  kwa wingi kuishangilia Stars siku ya Jumamosi kujenga dhana ya mchezaji wa 12 .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents