Burudani

Baada ya Alikiba, Rich Mavoko na wengineo Abydad kuibuka na Fid Q

Producer Aby Dad amesema siku si nyingi anakuja na ngoma ya raper Fid Q.

Aby Dad ambaye ametengeneza hit za wasanii kama Alikiba, Rich Mavoko, Kassimu Mganga na wengineo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa ana uwezo mkubwa katika kutengeneza muziki wa hip hop na si kwenye kuimba pekee.

“Nimeanza kugonga hip hop kabla hata ya hivi vitu vingine, kikubwa kaka zetu muziki huwa wanaujua vizuri japo wengi wanajua ninafanya muziki mmoja tu wa kuchezesha lakini kama mtu unafahamu muziki vizuri ukisikiliza nyimbo zangu nilizozitoa atajua kwa hichi ninachokisikia hata kitu fulani hawezi akashindwa” amesema Aby Day.

“Hip hop na hakika ni rahisi kuliko muziki ninaofanya mimi, kwa uwezo wangu binafsi Fid alifikiria nikienda pale kuna kitu tunaweza kukifanya, nimeshafanya naye ngoma ipo hapa time itakpofika nilitalizungumzia vizuri,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents