Michezo

Samatta kutua Premier League muda wowote, klabu 5 za England zamwania

Samatta kutua Premier League muda wowote, klabu 5 za England zamwania

Klabu ya Norwich City na Brighton zinazo shiriki ligi kuu England zimeanza kumuulizia mshambuliaji hatari wa KRC Genk na timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta.

Norwich and Brighton are believed to have enquired about Genk striker Mbwana Samatta

Licha ya timu hizo kuingia katika vita ya kutafuta saini ya nyota huyo wa Kimataifa wa Tanzania inaelezwa thamani yake ni pauni milioni 10.

Mbali na Norwich City na Brighton inadaiwa Samatta ambaye msimu huu tayari ameshatupia kambani jumla ya mabao 10 yakiwemo yale matatu kwenye michuano ya Champions League alipoifunga Liverpool na RB Salzburg lakini pia anawaniwa na timu ya Eintracht Frankfurt pamoja na Lazio.

The 27-year-old Tanzania international had also netted against Liverpool earlier this season

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 27, msimu uliyopita alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Ubelgiji akiwa na mabao 25 na kuisaidia Genk kutwaa taji huku akiiwezesha kucheza Champions League.

Hata hivyo Samatta, alitwaa tuzo ya Ebony Shoe akizawadiwa kama mchezaji bora kutoka Afrika hakika alikuwa na msimu mzuri.

Mshambuliaji huyo wa Taifa Stars amehusishwa pia kutaka kusajiliwa na klabu nyingi tu za England ambazo zinashiri Premier League zikiwemo Leicester, Aston Villa na Watford.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents