Bongo Movie

Shamsa amuumbua mwanamke anayemsumbua mume wake

Malkia wa filamu nchini, Shamsa Ford amedai kwamwe hata aachana na mume wake Chidi Mapenzi kisa mwanamke mwenzake.

Muigizaji huyo amesema hayo kwa madai kuna mwanamke anamletea figisu figisu mume wake.

“Nakupenda mume wangu halali wa ndoa aliyenipa mwenyezi Mungu. Sitoachana na wewe kwa ajili ya makelele ya wanadamu nitaachana na wewe kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Unanipenda, unaniheshimu, unajishusha kuomba msamaha pale unapokosea wakati wanaume wengine hawawezi kuomba msamaha hata wakikosea” aliandika Shamsa Instagram.

Aliongeza “Mume wangu nikikuelewa Mimi inatosha wengine wakipiga kelele tuchukulie kama burudani tu. Maana anajitahidi huyo anayeitwa ILALA MJINGA kama ulivyomsave kwenye simu yako kusambaza msg kwenye magroup na kuwatumia waandishi ushahidi. Jamani sitokuja kumuacha mume wangu kwa ajili ya mwanamke hata siku moja labda afanye makubwa yasiyoeleweka kwenye jamiii. Amecheat Bili clinton sembuse Rashid wangu ? Nakupenda RASHID WA SHAMSA FORD tupambane tuzidi kujenga familia yetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents