Michezo

Shinji Kagawa na Osako waing’arisha Japan michuano ya kombe la dunia

Timu ya taifa ya Japan imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya Colombia mchezo wa kundi H wa michuano ya kombe la dunia inayoendelea kutimua vumbi nchini Urusi.

Mabao ya Japan yakifungwa na kiungo wake anayekipiga klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Shinji Kagawa pamoja na Yuya Osako wakati la Colombia likifungwa na kiungo mshambuliaji, Juan Quintero ambaye anakipiga kwenye klabu ya River Plate kutoka nchini Argentine.

 

Kwa matokeo hayo Japan inatangulia kileleni mwa msimamo wa kundi hilo la H, huku ikisubiria mchezo wa Senegal na Poland.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents