Sio Rosa Ree tu, sitaki kushindanishwa na yeyote – Chemical

Rapper Chemical amesema moja ya vitu asivyovipenda ni kushindanishwa katika muziki.

Msanii huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Asali’ ameiambia ITV kuwa suala la kushindanishwa na Rosa Ree lingeanza wakati anatoka na ngoma zake kama Sielewi na VIP ila sio sasa.

“Sio Rosa Ree tu, sitaki ku-battle na mtu yeyote, mimi nafanya muziki wangu mwenyewe, ukitaka kushindana na mimi maana yake unaingia kwenye anga la Chemical, na ukiingia kwenye anga ya mtu huwezi kwa sababu kila mtu ana namna anavyopeleka muziki wake,” amesema.

“Nishatoa Sielewi mkaniona, nishatoa VIP mkaniona kabla hata ya huyo Rosa Ree, nilitoka kipindi kulikuwa hamna female rapper,” ameongeza Chemical.

Chemical kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya iitwayo Struggling wakati Rosa Ree anatamba na ngoma ‘Marathon’ aliyomshiirikisha Bill Nass.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW