Burudani

Snura amkingia kifua Shilole

Baada ya picha chafu za Shilole kusambaa mtandaoni hadi kupelekea baraza la sanaa la taifa, BASATA kumuandikia barua ya onyo, Snura amejitokeza na kumtetea.

11203450_826490997406450_1723893404_n

“Kiukweli kabla sijataka kusema itakuaje, mimi binafsi kutoka kwenye moyo wangu namuombea sana msamaha na Watanzania wasimuangalie hivyo ambavyo wanamuangalia,” Snura alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM.

“Ile ni kama ajali hivyo wamuelewe kama ambavyo mwenyewe amesema yule ni mtu mzima na ana maumivu yake ndani ya moyo kwa hiyo unapozidi kumkandamiza ni kama unazidi kumuumiza kikubwa ni kumsamehe na kuona je itatokea tena?” aliongeza.

“Siwezi kufurahia eti afungiwe ili iweje sawasawa Simba iombe Yanga ifungiwe unafikiri upinzani utakuja vipi kila kazi lazima awepo wakukupa changamoto naimani mie na Shilole tunapeana changamoto katika kazi yetu ni vizuri watanzania wamuelewe kuwa hiyo ni ajali tu katika kazi.”

Shilole na Snura ni wasanii wanaofananishwa na kupambanishwa mara nyingi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents