Michezo

Sportpesa kutoa Bajaji 100 kwa wateja wake kupitia promosheni ya #ShindanaSportPesa (+Video)

Kampuni ya kubashiri ya SportPesa, leo jumatano Oktoba 25 imezindua promosheni ya  ‘Shinda na SportPesa’ ambapo kwenye promosheni hiyo mshindi mmoja atashinda Bajaj moja aina ya TVS King mpya kwa siku na kutakuwa na Bajaj 100 zitakazotolewa kwa siku 100 kuanzia kesho.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba leo kwenye uzinduzi wa Promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA

Akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa Bakhresa, Manzese jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba amesema kuwa promosheni hiyo ina lengo la kubadili maisha ya Watanzania.

Sisi kama kampuni tumeona umuhimu wa kuja na promosheni hii ili kuweza kuwainua wateja kiuchumi na kuwaongezea mianya ya kujipatia kipato zaidi. Kama ulikuwa na TVS moja basi tutakuongezea ili uongeze kipato zaidi na kama ulikuwa huna kabisa basi tunakupa hii moja uanze leo.“amesema Bwana Abbas Tarimba.

Jinsi ya kushiriki kwenye promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA.

1-Kwanza ni lazima uwe mtumiaji wa SportPesa ili uweze kushinda Bajaj hiyo.

2-Kama bado hujajiunga na SportPesa au hujawahi kucheza na SportPesa. Tuma neno GAME kwenda 15888 na baada ya hapo utatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa kwa namba ya biashara 150888 na kumbukumbu namba 888, kisha piga *150*87# au tembelea www.sportpesa.co.tz kuweka utabiri wako (Kubeti) mara nyingi zaidi ili uweze kuingia kwenye droo.

3-Baada ya kucheza utatuma neno SHINDA kwenda 15888 na utakuwa umeingia kwenye droo kubwa ya kushindania Bajaj

Mbali na zawadi hiyo ya Bajaji kutakuwa na zawadi nyingine zitakazoshindaniwa ambazo ni Tiketi za kwenda nchini Uingereza kushuhudia mechi za EPL, Tiketi hizo zitatolewa kwa mshindi mmoja kwa kila mwezi na zawadi za jezi orijino za Arsenal na Everton ambazo zitatolewa kila wiki.

Mshindi wa Bajaji atatangazwa kila siku kuanzia kesho Alhamisi kupitia Clouds TV saa 1:30 Usiku.

Mfano wa Bajaj zitakazotolewa na SportPesa
Mabalozi wa SportPesa
Wadau wakifuatlia tukio hilo la uzinduzi
Wadau wakielekezwa namna ya kubeti na kujiunga na SportPesa ili washinde Bajaj.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents